BEKI wa kushoto wa Yanga, Nickson Kibabage ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kilichoweka kambi Tunisia tangu jana kujiandaa na mchezo wa mwisho wa Kundi F dhidi ya wenyeji, Algeria Septemba 7 kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Ivory Coast.
Kwa sasa Algeria ambayo imekwishafuzu inaongoza Kundi F kwa pointi 15, ikifuatiwa a Tanzania yenye pointi saba, wakati ina pointinne mbele ya Níger wanaoshika mkia kwapointi zao mbili.
Uganda itamaliza na Níger siku hiyo hiyo, Septemba 7 Uwanja wa Marrakech nchiniMorocco.
Tanzania imefuzu AFCON mara mbili tukihistoria, mwaka 1980 nchini Nigeria namwaka 2009 nchini Misri.
Kikosi cha Taifa Stars sasa ni; Makipa; Beno Kakolanya (Singida BS), Metacha Mnata (Yanga SC) na Erick Johola(Geita Gold).
Mabeki: Nickson Kibabage (Yanga), Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (Yanga SC), Bakari Mwamnyeto (Yanga SC), Dickson Job (Yanga SC), Kenedy Juma (Simba SC), Lameck Lawi (Coastal Union), Haji Mnoga(Aldershot Town, Uingereza), Abdi Banda (Richards Bay F.C, Afrika Kusini)
Viungo: Jonas Mkude (Yanga SC), MuzamilYassin (Simba SC), Sospeter Bajana (AzamFC), Himid Mao Mkami, (Tala’ea El Gaish, Misri), Mudathir Yahya, (Yanga SC), Abdulmalik Zakaria (Namungo FC), Maurice Abraham (FK Spotak Subotica, Serbia),Novatus Dismas (Zulte Waregem, Ubelgiji),
Washambuliaji: John Bocco (Simba SC), Clement Mzize (Yanga SC), Kibu Denis (Simba SC), Abdul Sopu (Azam FC), Ben Starkie (Basford United, Uingereza), Simon Msuva (JS Kabylie, Algeria) na Mbwana Samatta (PAOK FC, Ugiriki).
0 comments:
Post a Comment