TIMU ya Manchester City imefanikiwa kutwaa taji la UEFA Super Cup kwa mara ya kwanza katika histora yao baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Sevilla kufuatia sare ya 1-1 usiku wa jana Uwanja wa Georgios Karaiskáki mjini Athens nchini Ugiriki.
Sevilla, mabingwa wa UEFA Europa League walitangulia kwa bao la Youssef En-Nesryi dakika ya 25, kabla ya Cole Palmer kuwasawazishia Manchester City, mabingwa wa UEFA Champions League dakika ya 63.
Na katika mikwaju ya penalti, waliofunga za Man City ni Mnorway Erling Haaland, Muargentina Julián Álvarez, Mcroaria, Mateo Kovačić na Waingereza Jack Grealish na Kyle Walker, wakati za Sevilla zilifungwa na Muargentina, Lucas Ocampos, Mspaniola, Rafa Mir, Mcroatia Ivan Rakitić na Muargentina Gonzalo Montiel, huku Nemanja Gudelj pekee akikosa.
0 comments:
Post a Comment