MWENYEKITI wa Bodi ya Simba SC, Salim Abdallah Muhene 'Try Again' amehudhuria kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika jijini Sydney, Australia.
Akiwa huko, Try Again amepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino kuhusu Africa Super League na ushiriki wa Simba kwenye michuano hiyo pamoja na kuzungumzia mambo mengi yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na hasa Tanzania.
Rais Infantino amepongeza hatua kubwa ya maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika na zaidi Tanzania.
Ameipongeza pia Tanzania kwa kazi kubwa ambayo inafanyika katika kukuza mpira akifurahishwa zaidi Simba na vilabu vingine chini ya usimamizi mzuri wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).
0 comments:
Post a Comment