MABINGWA wa Tanzania,Yanga wamefanikiwa kwenda Raundi ya mwisho ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya AS Ali Sabieh (ASAS) ya Djibouti leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na winga Mkongo, Max Mpia Nzengeli dakika ya saba na 90 na ushei, mshambuliaji Mghana Hafiz Konkoni dakika ya 45, kiungo Muivory Coast Pacome Zouazoua na mshambuliaji chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Clement Mzize dakika ya 69, wakati bao pekee la ASAS limefungwa na Tito Mayor kwa penalti dakika ya 85.
Yanga inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 7-1 baada ya kuichapa AS Ali Sabieh 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita hapo hapo Azam Complex na sasa itakutana na Al-Merreikh ya Sudan mechi ya kwanza wakianzia ugenini Septemba 15 na marudiano na dar es Salaam Septemba 29.
0 comments:
Post a Comment