WACHEZAJI wapya wa Azam FC kutoka Senegal, beki Cheikh Sidibe na mshambuliaji Alasane Diao wameanza vizuri baada ya kufunga mabao katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan leo Uwanja wa Olimpiki mjini Rades nchini Tunisia.
Sidibe aliyesajiliwa kutoka Teungueth Rufisque alifunga bao la kwanza na Alasane Diao aliyesajiliwa kutoka US Goree za kwao, Senegal alifunga la tatu huku bao la pili likifungwa mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa kujipima nguvu kwa Azam katika wiki ya kwanza kati ya tatu ya kambi yake ya kujiandaa na msimu mpya katika Mji wa Sousse nchini Tunisia.
0 comments:
Post a Comment