MABAO ya Kibu Dennis na Nahodha, John Raphael Bocco yameipa Simba SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Turan FK ya Turkmenistan katika mchezo wa kirafiki leo mjini Ankara nchini Uturuki.
Huo ulikuwa nchezo wa pili wa kirafiki katika kambi yake ya kujiandaa na msimu nchini Uturuki baada ya sare ya 1-1 na Zira FK ya Azerbaijan Julai 24 na baadaye Saa 12:00 jioni timu hizo zitarudiana hapo hapo Ankara.
Turkmenistan ni nchi inayopatikana Asia ya Kati ikiwa imepakana na Kazakhstan upande wa Kaskazini Magharibi na Uzbekistan kwa Kaskazini Mashariki, ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 138 kwenye renki za FIFA ikiwa chini ya Tanzania ambayo ipo nafasi ya 123.
0 comments:
Post a Comment