KLABU ya Simba SC imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili kiungo Mtanzania, Abdallah Hamisi Riziki (24) kutoka Orapa United FC ya Botswana.
Huyo anakuwa mchezaji mpya wa tatu mzawa baada ya David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro na mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda aliyewahi kutamba Azam FC kabla ya kupelekwa kwa mkopo Tenerife ya Hispania.
Kwa ujumla Simba SC imesajili wachezaji wapya saba hadi sasa, wengine wanne ni wa kigeni wakiwemo Wacameroon wawili, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao na kiungo mshambuliaji, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
Wachezaji wengine wapya Simba ni kiungo Mkongo Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan, winga wa kushoto na Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment