KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji Mcameroon Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda kuwa mchezaji wake mpya wa kwanza kuelekea msimu ujao.
Onana mwenye umri wa miaka wa 22 anatua Simba SC baada ya misimu miwili ya kucheza Rayon Sports akiibuka mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Rwanda msimu uliopita 2022/2023.
Mpachika mabao huyo aliwasili Jijini Kigali mwezi Septemba mwaka 2021 akiwa sehemu ya wachezaji 50 waliojitokeza kufanya majaribio Rayon Sports chini ya kocha Juma Masudi.
Japokuwa kocha huyo Mrundi alifukuzwa kutokana na matokeo mabaya mwanzoni tu mwa msimu wa 2021/2022, aliwaacha Rayon Sports kifaa hicho ambacho kimegeuka kuwa tegemeo la klabu kwa misimu miwili.
Kabla ya kujiunga na Rayon Sports kwa majaribio 2021, nyota huyo anayetarajiwa pia kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Rwanda, alichezea Ending Sport FC ya kwao, klabu ambayo inasifika kwa kuibua vipaji vya chipukizi.
0 comments:
Post a Comment