SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa Ratiba ya michuano ya Ngao ya Jamii na mabingwa wa mataji yote nchini, Yanga SC watamenyana na Azam FC Agosti 9 huku Simba SC wakimenyana na Singida Fountain Gate Agosti 10 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mechi ya Fainali itafuatia Agosti 13 Saa 1:00 usiku ikitanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Saa 9:00 hapo hapo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment