KLABU ya Yanga imemtambulisha Msenegal, Moussa N'Daw kuwa kocha wake mpya Msaidizi akichukua nafasi ya Mrundi, Cedric Kaze aliyeondolewa.
Moussa N'Daw (54) ni Mwanasoka wa zamani wa Kimataifa wa Senegal, ambaye alikuwa mshambuliaji hodari enzi zake na alichezea klabu za Wydad Casablanca ya Morocco kati ya mwaka 1991 na 1992 kabla ya kuhamia Al-Hilal ya Saudí Arabia hadi mwaka 1994 alipokwenda Ureno kujiunga na Farense.
Mwaka 1999 alirejea Saudi Arabia alipojiunga na Al-Ittifaq hadi mwaka 2000 alipostaafu na kuanza kufundisha mpira klabu ya ASC Jeanne d'Arc ya kwao, Dakar.
0 comments:
Post a Comment