WAREMBO 20 wabaki vinywa wazi mara baada ya kutangazwa rasmi zawadi ya Miss Tanzania gari aina ya Mercedes benz yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 za Kitanzania pamoja na pesa taslim Milioni 10 kwa atakaeibuka Mshindi Usiku wa Leo katika ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Wanahabari wakati wa kutambulisha zawadi hiyo. Jijini Dar es salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa, amesema kuwa Fainali ya Miss Tanzania itapambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa warembo wenyewe huku akisisitiza kuwa Fainali hiyo itakuwa ya kitofauti kutokana na kupangika kwa matukio ya kiburudani zaidi.
"Nilipata nafasi ya kupita kambini kushuhudia mazoezi ya Fainali ya Miss Tanzania kutoka kwa washiriki wenyewe Kiukweli kuna hatari watu wanajifua namna ya kutembea jukwaani (catwalk) zaidi ya Mrembo Halima Kopwe (Miss Tanzania 2021) lipieni ving'amuzi mshuhudie burudani hiyo kupitia chaneli ya St bongo ndani ya Startimes. "
Malisa amewasihi watazamaji kulipia mapema ving'amuzi vyao ili kutazama mubashara Fainali hizo kwa wale ambao hawatabahatika kufika katika ukumbi wa the Superdome Masaki Jijini Dar es salaam.
Nae Meneja Mradi wa shindano hilo Ombeni Phiri amesema Washiriki hao 20 kutoka kanda mbalimbali wanaenda kugombania gari hiyo ambapo ni kwa mara ya pili mfululizo gari aina ya Mercedes benz kutolewa kwa mshindi.
"Warembo 20 wamekuwa kambi kwa siku 27 na kujifunza vitu mbalimbali hivyo sio jambo rahisi kwa warembo hao kuwa sehemu moja kutokana na kila mshiriki ana tabia yake.''
Hata hivyo Phiri amewatakia kila la heri warembo hao 20 kuelekea fainali hiyo ambapo mmojawapo anaenda kubadilisha maisha yake kupitia tasnia ya urembo na mitindo.
Hata hivyo kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Azam Mashango amesema washiriki wote 20 watapewa fedha kama kiinua mgongo isipokuwa Mshindi wa nne,tano na sita watapewa Milioni 1 ,Mshindi wa 3 milioni 2 huku Mshindi wa pili akipatiwa Milioni 2 na wa kwanza milioni 10 huku Mshindi wa 6 hadi 20 wakiambulia laki 2 kila mmoja.
Mashango amewapongeza wadau mbalimbali wa shindano hilo wakiwemo Robby One pharmacy, Startimes na wengine kuhakikisha shindano hilo linafanyika na linaonyeshwa mubashara kwenye King'amuzi hicho ili kuwapa nafasi wadau wa urembo kuwaona wasichana hao wadogo wenye kiu ya kutimiza ndoto zao kupitia tasnia ya urembo.
ORODHA YA WASHINDI WA TAJI LA MISS TANZANIA
2023 Halima Kopwe
2022 Juliana Rugumisa
2019 Sylvia Sebastian
2018 Queen Elizabeth Makune
2017 Julitha Kabete
2016 Diana Edward Lukumay
2015 Lilian Kamazima
2014 Happiness Watimanywa
2013 Brigitte Alfred Lyimo
2012 Lisa Jensen
2011 Salha Kifai
2010 Genevieve Emmanuel Mpangala
2009 Miriam Gerald Unplaced
2008 Nasreen Karim
2007 Richa Adhia
2006 Wema Sepetu
2005 Nancy Sumari
2004 Faraja Kotta
2003 Sylvia Bahame
2002 Angela Damas
2001 Happiness Magese
2000 Jacqueline Ntuyabaliwe
1999 Hoyce Temu
1998 Basila Mwanukuzi
1997 Saida Kessy
1996 Shose Sinare
1995 Emily Adolf
1994 Aina Maeda
1967 Theresa Shayo
0 comments:
Post a Comment