KLABU ya Tanzania Prisons ya Mbeya imemtambulisha Freddy Félix Minziro kuwa kocha wake mpya Mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Geita Gold.
Freddy Félix Minziro, beki wa zamani wa Yanga, kutua Tanzania Prisons ni sawa na kurejea nyumbani, kwani ni klabu ambayo aliifundisha mara kadhaa kuanzia miaka ya 1990.
0 comments:
Post a Comment