KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo wa Kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fabrice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan kuwa mchezaji wake mpya wa sita kuelekea msimu ujao.
Wachezaji wengine wapya Simba SC ni beki mzawa, David Kameta ‘Duchu’ kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, beki wa katí Che Fondoh Malone Junior kutoka Cotton Sport ya kwao, Cameroon, winga wa kushoto, Aubin Kramo Kouamé kutoka ASEC Mimosas ya kwao, Ivory Coast na mshambuliaji Mcameroon, Leandre Essomba Willy Onana kutoka Rayon Sport ya Rwanda.
Fabrice Luamba Ngoma (29) ni kiungo mzoefu aliyeibukia klabu ya Sharks XI mwaka 2014, kabla ya kuhamia MK Etanchéité mwaka 2015 zote za DRC.
Mwaka 2017 akahamia Ifeanyi Ubah ya Nigeria kabla ya mwaka 2019 kurejea nyumbani kuchezea AS Vita Club hadi 2022 alipohamia Raja CA ya Morocco na 2022 Al-Fahaheel SC ya Kuwait kabla ya mapema mwaka huu kutua Al-Hilal.
0 comments:
Post a Comment