KLABU ya Azam FC imemtambulisha beki wa kushoto wa kimataifa wa Senegal, Cheikh Tidiane Sidibe kutoka Teungueth ya kwao.
“Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeinasa saini ya beki wa kushoto wa kimataifa wa Senegal, Cheikh Tidiane Sidibe, akisaini mkataba wa miaka miwili akitokea Teungueth,” imesema taarifa ya Azam.
Cheikh Tidiane Sidibe (24) ambaye ni hodari kwa kusaidia mashambulizi na kupiga mipira ya adhabu ndogo anakuwa mchezaji wa nne mpya Azam FC baada ya viungo mzawa, Feisal Salum, Mgambia Djibril Sillah na mshambuliaji Alassane Diao kutoka Senegal pia.
0 comments:
Post a Comment