KLABU ya Azam FC kesho imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, US Monastir katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Mustapha Ben Jannet mjini Monastir nchini Tunisia.
Mabao ya Azam FC iliyoweka kambi mjini Sousse nchini Tunisia kujiandaa na msimu yamefungwa na viungo Mghana, James Akaminko dakika ya 13 na Mguinea Djibril Sillah dakika ya 39 baada ya Monastir kusawazisha.
Huo ni mchezo wa tatu wa kirafiki kwa Azam FC kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mjini Sousse nchini Tunisia baada ya awali kushinda 3-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan Julai 14 na kufungwa 3-0 na wenyeji, Esperance Julai 19.
0 comments:
Post a Comment