TIMU ya Azam FC jana imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa mara ya pili mfululizo.
Hiyo ni kufuatia sare tasa ya wapinzani wao wa karibu, Yanga SC dhidi ya Mbeya Kwanza jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam baada ya Azam FC kushinda 4-0 dhidi ya African Sports, katika mchezo uliotangulia.
Azam FC iliingia kwenye mchezo huo ikiwa mbele kwa pointi tatu dhidi ya Yanga na baada ya matokeo ya jana sasa inaongoza kwa pointi tano kuendelea mechi moja moja za mwisho.
0 comments:
Post a Comment