KLABU ya Azam Jumatano itacheza mechi ya pili ya kujipima nguvu katika kambi ya kujiandaa na msimu mpya nchini Tunisia dhidi ya wenyeji, Esperance ya Jijini Tunis.
Mchezo huo ulikuwa ufanyike Uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo, Park Esperance, lakini, wenyeji hao wametuma maombi kwenye Serikali yao ufanyike Uwanja wa Taifa wa Rades.
Julai 27 mwaka huu, Esperance watacheza na Al Ittihad Jeddah ya Saudi Arabia iliyowasajili Karim Benzema na N'Golo Kante kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Mataifa ya kiarabu.
Kwa Azam, huo utakuwa mchezo wa pili ya kirafiki kwenye kambi yao mjini Sousse, Tunisia baada ya kuichapa Al Hilal ya Sudan 3-0 Julai 14 mabao ya Wasenegal Cheikh Sidibe, Alassane Diao na Mzimbabwe Prince Dube.
0 comments:
Post a Comment