KLABU ya Yanga imeachana na winga Dickson Ambundo baada ya misimu miwili ya kuwa na timu hiyo tangu akizungumza nayo kutoka Dodoma Jiji FC.
Dickson Ambundo anakuwa mchezaji wa tatu kuondoka Yanga kutoka kikosi cha msimu uliopita baada ya kiungo Mzanzibari Feisal Salum aliyeuzwa Azam FC na winga mwingine, Mkongo Tuisila Kisinda.
“Tunamshukuru Ambundo kwa mchango wake katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya Young Africans SC,”imesema taarifa ya Yanga jioni hii.
Tayari Yanga imeachana na Kocha wake Mkuu, Mtunisia Nasredeen Nabi na Kocha wa makipa, Mbrazil Milton Nienov.
0 comments:
Post a Comment