WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana Juni, 2, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika ( CAF), Veron Mosengo Omba jijini Algiers nchini Algeria.
Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Algeria Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, ambapo Pindi amemshukuru kwa kupokea andiko (bid) la maombi ya Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa kwa pamoja mashindano ya AFCON mwaka 2027.
Pindi pia amemuhakikishia Bw. Veron kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha inaandaa miundombinu ya kisasa yenye viwango vya Kimataifa kwa lengo la kukidhi vigezo vya CAF vya kuandaa mashindano hayo.
Veron ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa shughuli za michezo.
0 comments:
Post a Comment