KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Abdul Suleiman Sopu amefunga mabao matatu kuipa Timu ya marafiki wa Mbwana Samatta ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Marafiki wa mwanamuziki Ally Kiba leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo wa Hisani kwenye Tamasha la Sama Kiba, linalojulikana pia kama Nifuate Sopu amefunga mabao yake dakika za 45,63 na 71, wakati la lingine limefungwa na Nahodha wa Simba, John Bocco dakika ya 21.
Mabao ya Team Kiba yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ayoub Lyanga dakika ya 69 na mwanamuziki Omary Ally Mwanga ‘Mario’ dakika ya 90 na ushei.
Samatta, mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji amekuwa akishirikiana na mwanamuziki Ally Kiba kufanya tamasha hilo la hisani kwa Hisani kwa miaka sita sasa.
0 comments:
Post a Comment