KLABU ya Simba imetangaza kuachana na kiungo mkongwe anayeweza kucheza nafasi zote za ulinzi katikati na pembeni, Erasto Edward Nyoni baada ya kuitumikia timu tangu mwaka 2017 aliposajiliwa kutoka Azam FC.
Erasto Nyoni anakuwa mchezaji wa sita kuachwa Simba baada ya kipa Beno Kakolanya, beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Wanigeria, Nelson Okwa, Víctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah.
Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula.
0 comments:
Post a Comment