VIGOGO, Simba na Yanga wameendelea kuboronga katika Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya wote kufungwa katika mechi za leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Yanga SC imechapwa 3-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Kundi B mabao ya washindi yakifungwa na Emanuel Mbogo, Kelvin Sengati na Iddy Kichindo huku bao pekee la ‘Makinda ya Jangwani’ likifungwa na Ladius Lucas.
Mechi nyingine ya Kundi B timu za Dodoma Jiji na Polisi Tanzania zimetoka sare ya 2-2. Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Edward Maliganya na John Nyamba na ya Polisi Tanzania yamefungwa na Crespo Haule na Baraka Mwambe aliyejifunga.
Nayo Simba imechapwa 1-0 na Ihefu SC bao pekee la Ben Ng’wani, wakati Azam FC imeshinda 1-0 dhidi ya Kagera Sugar bao pekee la Cyprian Kachwele katika mechi za Kundi D.
Mechi za kwanza Yanga ilichapwa 1-0 na Dodoma Jiji, wakati Simba ilitoka sare ya 0-0 na Kagera Sugar na Azam FC iliichapa Ihefu 1-0 na Prisons iliichapa Polisi Tanzania 4-2.
0 comments:
Post a Comment