// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAKHO AITWA TIMU YA TAIFA SENEGAL KUIVAA BRAZIL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAKHO AITWA TIMU YA TAIFA SENEGAL KUIVAA BRAZIL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, June 02, 2023

    SAKHO AITWA TIMU YA TAIFA SENEGAL KUIVAA BRAZIL


    KOCHA wa Senegal, Aliou Cissé  amemjumuisha kwenye kikosi chake winga wa Simba SC, Pape Ousmane Sakho kwa ajili ya mbili mwezi huu dhidi ya Benín Juni 17 na Brazil Juni 20 zote ugenini.
    Mechi dhidi ya Benín ni ya Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani ambazo wao Ivory Coast ndio wenyeji na ya Brazil ni ya kirafiki ambayo itapigwa Uwanja wa José Alvalade Jijini Lisbon nchini Ureno.
    Senegal imekwishajihakikishia tiketi ya AFCON ya mwakani ikiwa inaongoza Kundi L kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Msumbiji pointi nne, Rwanda tatu na Benín mbili kuelekea mechi mbili za mwisho.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAKHO AITWA TIMU YA TAIFA SENEGAL KUIVAA BRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top