MABINGWA watetezi, Mtibwa Sugar wameanza vyema Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ezekiel Eusebio mawili, Athumani Makambo, Said Salum na Said Mkopi.
Mechi nyingine ya Kundi A leo Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Namungo FC hapo hapo, huku mechi za Kundi C Geita Gold ikiilaza KMC 2-0 na Coastal Unión ikiichapa Singida Big Stars 1-0 hapo hapo Chamazi.
Kesho ni mechi za Kundi B Polisi na Tanzania Prisons Saa 8:00 mchana, Yanga na Dodoma Jiji Saa 10:15 jioni na za Kundi D Simba na Kagera Sugar Saa 12:30 jioni na Azam FC na Ihefu Saa 2:45 usiku.
0 comments:
Post a Comment