KOCHA Mtunisia wa Yanga, Nasredine Mohamed Nabi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake kwenye klabu hiyo na sekta ya michezo kwa ujumla.
Nabi amesema hayo baada ya mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Shujaa wa Yanga leo ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 14 akimalizia kazi nzuri ya beki Mkongo, Djuma Shabani.
Pamoja na ubingwa wa Ligi Kuu na ASFC, Yanga pia ni washindi wa Ngao ya Jamii na washindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika, wakihitimisha msimu mzuri kwao kihistoria chini ya kocha Nabi.
0 comments:
Post a Comment