NCHI Wanachama wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV zimeichagua Tanzania kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza hilo linaloundwa na nchi 14.
Ushindi huo umepatikana kupitia mkutano wa Baraza hilo uliofanyika leo Mei 4, 2023 jijini Arusha chini ya uongozi wa na Mwenyekiti Mhe.Peter Ogwang ambaye ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Michezo nchini Uganda.
Tanzania imepitiswa na Wajumbe kutoka Nchi 14 zinazoshiriki Mkutano huo ambazo ni Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Shelisheli, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Uganda na wenyeji Tanzania.
Akizungumza mara baada ya Tanzania kuchaguliwa, Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewashukuru Wajumbe hao akiwahakikishia kuwa Tanzania itakua tayari kusimamia, kuendeleza na kuhakikisha mipango na matarajio ya Baraza hilo yanafikiwa kwa mafanikio makubwa.
Mkutano unaofuata wa Baraza hilo utafanyika Zanzibar Aprili mwakani.
0 comments:
Post a Comment