TANZANIA itaanza na Kongo katika Raundi ya Kwanz aya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Michezo ya Olimpiki (WOFT) Paris 2024 nchini Ufaransa.
Ikifanikiwa kuitoa Kongo, Tanzania itakutana na mshindi kati ya Msumbiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Jumla ya timu 25 zimeingia kwenye mchujo wa kuwania tiketi ya Olimpiki mwakani, huku 18 zikienda moja kwa moja Raundi ya Kwanza na saba zilizobaki zikiongozwa na mabingwa, Afrika Kusini ambazozipo nafasi za juu kwenye renki baada ya Fainali za Kombe la Mataifa ya afrika mwaka jana (WAFCON) zitaanzia Raundi ya Pili.
Washindi tisa wa Raundi ya Kwanza zitaungana na saba za renki za juu kwa ajili ya Raundi ya Pili itakayohusisha timu 16 na washindi nane watasonga Raundi ya Tatu, kisha nne zitamenyana katika Raundi ya Nne.
Washindi wawili wa Raundi ya Nne watafuzu kwenye Fainakli ya Michezo ya ya Paris mwakani.
Kwenye Olimpiki ya mwaka jana Jijini Tokyo nchini Japan, Zambia iliiwakilisha Afrika, na sasa She-polopolo wataanza kampeni yao ya kufuzu mfululizo katika Raundi ya Pili.
Mechi za Raundi ya Kwanza zitachezwa kati ya Julai 10 na 18 2023, Raundi ya Pili Oktoba 23 hadi 31, Raundi ya Tatu Februari 19 hadi 28, 2024 wakati Raundi ya mwisho itafuata Aprili 1 hadi 9, 2024.
RAUNDI YA KWANZA (Julai 10–18, 2023)
Guinea Bissau vs Benin, Guinea vs Ghana, Burkina Faso vs Mali, Cote d’Ivoire vs Sierra Leone, Namibia vs Equatorial Guinea, Uganda vs Rwanda, Ethiopia vs Chad, Congo vs Tanzania, Mozambique vs DR Congo.
RAUNDI YA PILI (Oktoba 23–31, 2023)
Guinea Bissau/Benin vs Guinea/Ghana, Burkina Faso/Mali vs Zambia, Cote d’Ivoire/Sierra Leone vs Tunisia, Namivia/Equatorial Guinea vs Morocco, Uganda/Rwanda vs Cameroon, Ethiopia/Chad vs Nigeria, Congo/Tanzania vs Botswana, Mozambique/DR Congo vs South Africa.
(Raundi ya Tatu Februari 19–28, 2024 na Raundi ya Nne Aprili 1–9 April 2024)
0 comments:
Post a Comment