• HABARI MPYA

        Friday, May 19, 2023

        FAINALI EUROPA LEAGUE NI ROMA YA MOURINHO NA SEVILLA


        TIMU ya AS Roma imefanikiwa kutinga Fainali ya Europa League baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Bayer Leverkusen kwenye mchezo wa marudiano wa Nusu leo usiku wa Alhamisi Uwanja wa BayArena Jijini Leverkusen.
        Timu hiyo ya kocha Mreno, José Mourinho inanufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Italia na sasa itakutana na Sevilla iliyoitoa Juventus.
        Sevilla imeitoa Juventus kwa jumla ya mabao 3-2 kufuatia ushindi wa 2-1 jana Hispania ikitoka kutoa droo ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Italia.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: FAINALI EUROPA LEAGUE NI ROMA YA MOURINHO NA SEVILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry