TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba SC leo Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1, Azam FC wakitangulia kwa bao la Lusajo Mwaikenda dakika ya 22, kabla ya kiungo wa Mali, Sadio Kanoute kuisawazishia Simba dakika ya 27.
Shujaa wa Azam FC leo ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo aliyefunga bao la ushindi dakika ya 74 kufuatia kuingia dakika ya 69 kuchukua nafasi ya Mkongo, Idris Mbombo aliyeumia.
Simba ilimaliza pungufu baada ya Kanoute kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 86 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Azam FC sasa itakutana na mshindi kati ya Singida Big Stars na Yanga ambazo zitamenyana baadaye mwezi huu.
0 comments:
Post a Comment