KUELEKEA pambano la watani Jumapili, beki Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba ametoa pasi tano za mabao, huku beki mwenzake wa kushoto, Joyce Lomalisa Mutambala wa Yanga akiwa ametoa nne tu.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara kutoka Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB), kipa Mmali, Djigui Diarra wa Yanga anamzidi Clean Sheets tatu mlinda mlango namba moja nchini, Aishi Salum Manula.
Kwa upande wa washambuliaji, Mzambia Moses Phiri wa Simba amefunga mabao 10 na assists tatu, Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele ana mabao 16 na assists mbili.
0 comments:
Post a Comment