// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TIMU ZA TAIFA NDONDI WANAWAKE NA WANAUME ZATEULIWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TIMU ZA TAIFA NDONDI WANAWAKE NA WANAUME ZATEULIWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, April 07, 2023

    TIMU ZA TAIFA NDONDI WANAWAKE NA WANAUME ZATEULIWA


    SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) Aprili 5 lilifanya mashindano ya mchujo na kupata mabondia watakao wakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya kanda ya tatu Afrika yatakayofanyika uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) tarehe 18-22 Aprili 2023. 
    Kwa mujibu wa Makore Mashaga, Katibu Mkuu Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), mashindano hayo yatashirikisha nchi 14 wanachama wa kanda ya tatu.
    Amesema mchujo huo umefanyika katika ukumbi wa mazoezi wa timu ya ngumi ya JKT Mgulani. Jumla ya mabondia 22, ikiwa wanaume 16 na wanawake 6 ndio waliochagulia miongoni mwa mabondia 56 walikuwa katika maandalizi ya mashindano hayo.
    Amesema mabondia waliochaguliwa ni wale walionyesha uwezo mzuri kuwashinda wenzao kutoka katika kambi tatu tofauti zilizokuwa zikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo kutoka katika kambi za timu ya ngumi ya Ngome, timu ya ngumi ya Magereza na timu ya ngumi ya JKT Mgulani.
    Mashaga amesema kwa sasa mabondia waliochaguliwa watafanya mazoezi katika kituo kimoja JKT Mgulani.
    Ameongeza kwamba Kamati ya BFT imechagua kituo hicho kutokana na kuwepo kwa miundo mbinu mizuri ya kuwezesha kufanya mazoezi ya ngumi kwa ufanisi kwa maandalizi ya mwisho na ya pamoja.
    Amesema nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kongo Brazzaville, Afrika ya Kati, Gabon, Cameroon na Equatorial Guinea.
    Aidha, Mashaga amewataha mabondia waliochaguliwa kuunda timu za taifa za Tanzania kwa wanaume, wanawake, Makocha na kamati ya ufundi pia kwa ajili ya mashindano hayo.
    ORODHA YA MABONDIA WA KIUME WALIOCHAGULIWA TIMU YA TAIFA
    Karim Juma - Minimume
    Yohana Keneth - Fly
    Abdalah Salum - Bantam
    Hassan Waziri - Feather
    Rashid Mrema - Light
    Alex Isendi - Light Welterweight
    Mohamed Swalahe - Light Welter
    Atanas Ndiganya - Welter
    Joseph Phillip - Light Middle
    David Chanzi - Middle
    Joshua Shadrack - Middle
    Alphonce Abel - Middle
    Yusuf Changalawe - Light Heavy
    Nizza Abdalahamani - Light Heavy
    Jofrey Peter - Cruser
    Alex Sitta - Super Heavy
    ORODHA YA MABONDIA WA KIKE WALIOCHAGULIWA TIMU YA TAIFA
    Rahma - Minimum
    Mariam Richard - Light Flyw
    Shakila Abdalah - Fly
    Aisha Iddi - Bantam
    Leila Yazidu - Bantam
    Beatrice Ambrose - Light
    MAKOCHA
    1. Samwel Batman – (IBA 1 Star)
    2. Hassan Mzonge
    3. Mussini Mohamed
    4. Rogata Damian (IBA 1 Star)
    5. Undule Lang’son
    6. Haji Abdalah
    KAMATI YA UFUNDI
    1. Michael Changarawe – Mwanza
    2. Robert Sululu – Dar es salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU ZA TAIFA NDONDI WANAWAKE NA WANAUME ZATEULIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top