// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAFA KIUME MOROCCO, YATOLEWA KWA MATUTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAFA KIUME MOROCCO, YATOLEWA KWA MATUTA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, April 29, 2023

    SIMBA SC YAFA KIUME MOROCCO, YATOLEWA KWA MATUTA


    SAFARI ya Simba SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara nyingine leo imeishia hatua ya Robo Fainali baada ya kutolewa na mabingwa watetezi, Wydad Club Athletic kwa penalti 4-3 usiku huu Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Morocco.
    Dakika 90 zilimalizika kwa Wydad AC kushinda 1-0, bao pekee la mshambuliaji Msenegal, Bouly Junior Sambou dakika ya 24 kwa kichwa na kufanya sare ya jumla ya 1-1 kufuatia Simba kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita Dar es Salaam, bao la mshambuliaji Mkongo Jean Othos Baleke dakika ya 31.
    Na katika mikwaju ya penalti, shujaa wa Wydad alikuwa ni kipa Youssef El Motie ayeokoa penalti mbili za beki Shomari Kapombe na kiungo Clatous Chama.
    Waliofunga penalti za Wydad ni kiungo Yahya Jabrane, mabeki Ayoub El Amloud, Amine Aboulfath na kiungo Abdellah Haimoud wakati waliofunga za Simba ni viungo Erasto Nyoni, Mrundi Said Ntibanzokiza na mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri.
    Sasa Wydad itakutana na mshindi wa jumla katí ya CR Belouizdad ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zinazorudiana Jumamosi Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria. 
    Mechi ya kwanza Mamelodi ilishinda 4-1 Uwanja wa Nelson Mandela mjini Baraki, Algiers, Algeria.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YAFA KIUME MOROCCO, YATOLEWA KWA MATUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top