NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema kwamba Serikali inaangalia upya utaratibu ambao utawezesha klabu kunufaika zaidi na mapato ya milangoni katika mechi.
Mwinjuma amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Iramba Mashariki, Francis Mtinga kuhusu Mgawanyo wa mapato uliotolewa kwenye mechi iliyowakutanisha Simba na Yanga Aprili 16,2023.
Mtinga amehoji ni lini Serikali itapitia upya utaratibu wa mgawanyo wa mapato baada ya Simba kupewa Shilingi Milioni 180 pekee kati ya Miliomi 450 zilizopatikana kwenye mchezo dhidi ya Yanga.
“Tunaangalia utaratibu ambao utawezesha vilabu vyetu kunufaika zaidi, lakini kuna gharama kubwa za uendeshaji wa michezo inayotajwa na taasisi zetu zinaingia gharama kubwa ambayo inatoka mifukoni kwao kuweza kuifanya michezo hii ifanikiwe,”.
“Kwa hiyo pamoja na lengo letu la kuhakikisha timu zetu zinafaidika lakini kuna gharama kubwa za uendeshaji na taasisi zetu zitashindwa kujiendesha kama tutazizuia kukata makato yao,” amesema Naibu Waziri Mwinjuma.
0 comments:
Post a Comment