TANZANIA PRISONS YAICHAPA RUVU SHOOTING 3-1 SOKOINE
WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Jumanne Elfadhil dakika ya sita na Jeremiah Juma, mawili dakika ya 41 na 50, baada ya Valentino Mashaka kuanza kuifungia Ruvu Shooting dakika ya pili. Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons inafikisha pointi 28 na kusogea nafasi ya 10, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 20 nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi 26. Ikumbukwe mwishoni mwa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja, wakati watakaomaliza nafasi ya 13 na 14 watamenyana baina yao timu itakayofungwa baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini itakwenda kucheza timu ya Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
Coach Botes trims Teen Cranes Squad to 25
-
Uganda U17 Women’s National Football Team Coach Sheryl Botes Ulanda, has
today trimmed the number to 25 players that will continue preparing for the
CAF ...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment