MABAO ya James Ambroce na Mashaka Hamisi yamewapa wenyeji, Pamba FC ushindi wa 2-0 dhidi ya Mashujaa katika mchezo wa Ligi ya Championship leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Mechi nyingine za Championship leo, vinara JKT Tanzania wameichapa African Sports 2-0 Jijini Tanga, Ken Gold wameichapa Green Warriors 2-1 na Mbuni FC wameitandika Fountain Gate 4-1.
Kwa ushindi huo, Pamba FC inafikisha pointi 51 na kupanda nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja Kitayosce FC baada ya wote kucheza mechi 24, wakiwa nyuma ya JKT Tanzania yenye pointi 62 za mechi 25.
Ikumbukwe timu mbili za huu zitapanda moja kwa moja Ligi Kuu na zitakazomaliza nafasi ya tatu na ya nne zitamenyana zenye we kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atakwenda kumenyana na timu ya Ligi Kuu kuwania kupanda.
Timu ya Ligi Kuu itayocheza na timu ya Championship ni ile itakayofungwa baada ya mechi mbili za timu baina ya timu za nafasi ya 13 na 14 Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment