KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesgeza mbele usikilizaji wa ombi la kiungo Feisal Salum kuomba kuvunja mkataba na Yanga hadi Mei 4, mwaka huu.
Taarifa ya Kamati haikusema sababu, lakini Wakili wa Yanga, Simon Patrick amesema imetokana na pingamizi walilowasilisha.
Wakili Patrick alisema baada ya Kamati hiyo awali kuamua Feisal ni mchezaji halali wa Yanga alitakiwa kuripoti klabuni na kama ana ombi la kutaka aondoke awasilishe.
Hata hivyo, Wakili Patrick amesema Feisal hakutaka kurejea klabuni wala kufanya taratibu zozote za kuomba kuvunja mkataba.
Ikumbukwe Feisal amesusa kufanya kazi Yanga tangu Januari akishinikiza kuondoka, lakini mkataba aliosaini ambao unamalizika mwakani ndio umekuwa kikwazo licha ya kupeleka kesi hadi TFF.
0 comments:
Post a Comment