KIUNGO wa Yanga SC, Mudathir Yahya Abbas ameingia kwenye kinyanga’nyiro cha kuwania ushindi wa Bao Bora kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mudathir ameingia kutokana na bao lake alilofunga kwenye mechi ya ushindi wa 3-1 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Februari 19, mwaka huu Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Lilikuwa bao la pili katika mchezo huo alilofunga dakika ya 11 akimalizia pasi ya mfungaji wa bao la kwanza, mshambuliaji Kennedy Musonda, wakati bao la tatu la Yanga lilifungwa na kiungo Mkongo, Tuisila Kisinda dakika ya 90 na ushei.
Muda atachuana na wachezaji wengine waliofunga dhidi ya timu za DRC pia, Aymen Mahious wa USM Alger kwa bao alilofunga dhidi ya St. Eloi Lupopo, Aubin Kramo Kouamé wa ASEC Mimosa ya Ivory Coast kwa bao alilofunga dhidi ya Diables Noirs pia na Paul Acquah wa Rivers United kwa bao alilowafunga DC Motema Pembe.
0 comments:
Post a Comment