MSHAMBULIAJI wa Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele jana amefikisha mabao 16 baada ya kufunga bao moja kwenye ushindi wa 5-0 wa timu yake dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Maana yake Mayele amefikia rekodi ya msimu uliopita kumaliza na mabao 16 na kushika nafasi ya pili kwa Ufungaji Bora nyuma ya George Mpole aliyekuwa Geita Gold.
Msimu huu Mayele yupo kwenye nafasi nzuri ya kuwa mfungaji bora, kuelekea mechi tano za mwisho, kwani hadi sasa wanaomfuatia Moses Phiri na Saido Ntibanzokiza wote wa Simba SC kila mmoja ana mabao 10.
Wengine wanaomfukuzia Mayele ni Nahodha wa Simba, John Bocco mwenye mabao tisa sawa na Mbrazil, Bruno Gomes wa Singida Big Stars na Sixtus Sabilo wa Mbeya City.
0 comments:
Post a Comment