WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Bayern Munich katika Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumanne Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Man City yamefungwa na Rodri dakika ya 27, Bernardo Silva dakika ya 70 na Erling Haaland dakika ya 76 kocha Pep Guardiola akiiadhibu timu yake ya zamani.
Manchester City watasafiri hadi Ujerumani kwa mchezo wa marudiano Aprili 19 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich.
Mechi nyingine ya Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa leo Ínter Milán wameshinda 2-0, dhidi ya wenyeji, Benfica nchini Ureno mabao ya Nicolò Barella dakika ya 51 na Romelu Lukaku kwa penalti dakika ya 82 na wao pia watatudiana Aprili 19 Italia.
0 comments:
Post a Comment