TIMU ya Sevilla imetoka nyuma na kutoa sare ya 2-2 na wenyeji, Manchester United katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford, Manchester.
Mabao ya Manchester United yalifungwa na Marcel Sabitzer yote dakika za 14 na 21, wakati ya Sevilla yalifungwa na mabeki Tyrell Malacia dakika ya 84 na Harry Maguire aliyejifunga dakika ya 90 na ushei.
Timu hizo zitarudiana Aprili 20 Uwanja wa Ramón Sánchez Pizjuán mjini Sevilla na mshindi wa jumla atakwenda Nusu Fainali.
Mechi nyingine za jana za kwanza za Robo Fainali Europa League Feyenoord imeichapa Roma 1-0, Juventus imeichapa Sporting Lisbon 1-0 na Bayer Leverkusen imetoa sare ya 1-1 na Union Saint-Gilloise.
0 comments:
Post a Comment