// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KOCHA NABI AREJEA YANGA BAADA YA KUKOSEKANA WIKI MBILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KOCHA NABI AREJEA YANGA BAADA YA KUKOSEKANA WIKI MBILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 10, 2023

    KOCHA NABI AREJEA YANGA BAADA YA KUKOSEKANA WIKI MBILI


    KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Mtunisia Nasredine Nabi amerejea nchini baada ya mapumziko ya wiki mbili na leo ameanza kuinoa timu kuelekea mechi na Kagera Sugar keshokutwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
    Nabi hakuwepo Yanga ikipata ushindi mwembamba wa 1-0 mara mbili katika mechi mbili zilizopita ugenini na nyumbani katika michuano tofauti.
    Kwanza ni ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, TP Mazembe kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika Jijini Lubumbashi Aprili 2 na baadaye Jumamosi dhidi ya Geita Gold katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu Azam Sports Federation Cup (ASFC). 
    Baada ya mchezo wa Jumanne na Kagera Sugar Yanga itarejea kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya watani, Simba SC Aprili 16.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA NABI AREJEA YANGA BAADA YA KUKOSEKANA WIKI MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top