MSHAMBULIAJI Erling Haaland amevunja rekodi ya mabao katika mechi 38 za msimu wa Ligi Kuu ya England baada ya kufunga bao la 33 kwenye ushindi wa Manchester City dhidi ya Arsenal Jumatano.
Mnorway huyo amekuwa wa moto katika msimu wake wa kwanza akifukuza rekodi England iliyowekwa na nyota wa Liverpool, Mohamed Salah.
Mmisri huyo amekuwa akishikilia rekodi hiyo tangu msimu wa 2017-18, alipofunga mabao 32, kabla ya kuwasili kwa Haaland.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alifikia rekodi ya Salah katika ushindi wa Man City wa 3-1 dhidi ya Leicester mwezi huu, kabla ya kuipita kwa bao la dakika za Lala salama dhidi ya Arsenal.
REKODI YA MABAO KWENYE MECHI 38 LIGI KUU ENGLAND
33 - Erling Haaland (2022-23)
32 - Mohamed Salah (2017-18)
31 - Luis Suárez (2013-14)
31 - Cristiano Ronaldo (2007-08)
31 - Alan Shearer (1995-96)
0 comments:
Post a Comment