MABINGWA watetezi, Manchester City jana wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad, Manchester.
Mabao ya Manchester City jana yamefungwa na John Stones dakika ya tano na Erling Haaland dakika ya 13 na 25, wakati la Leicester City limefungwa na Kelechi Iheanacho akiiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 75.
Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 70, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 30, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 25 za mechi 31 nafasi ya 19.
0 comments:
Post a Comment