KIPA wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra wa Yanga jana alifikisha mechi 15 za kusimama langoni bila kuruhusu bao, timu yake ikiibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Diarra aliye katika msimu wake wa pili Yanga sasa anendelea kuongoza miongoni mwa makipa wa Ligi Kuu kwa kudaka mechi nyingi bila kufungwa, akifuatiwa na Aishi Salum Manula wa Simba SC mwenye mechi 12 za kutoruhusu bao na Mcomoro wa Azam FC, Ali Ahamada mwenye mech nane.

0 comments:
Post a Comment