• HABARI MPYA

        Monday, March 20, 2023

        SINGIDA BIG STARS KUWEKA KAMBI TUNISIA


        KLABU ya Singida Big Stars itakwenda kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao nchini Tunisia kwa ufadhili wa wenyeji, US Monastir.
        Hiyo ni baada ya leo uongozi wa Singida Big Stars kuingia mkataba wa ushirikiano na US Monastir katika masuala ya utawala, uendeshaji na ufundi.
        Ni katika makubaliano hayo Singida Big Stars imepewa ofa maalum ya kuweka kambi ya maandalizi (Pre Season) ya msimu wa 2023/24 nchini Tunisia ambapo tutatumia Viwanja, Hoteli na rasilimali nyingine kwa hisani ya US Monastir.


        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS KUWEKA KAMBI TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry