// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SERIKALI YAWAAHIDI SH MILIONI 500 TAIFA STARS WAKIFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SERIKALI YAWAAHIDI SH MILIONI 500 TAIFA STARS WAKIFUZU AFCON - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 20, 2023

    SERIKALI YAWAAHIDI SH MILIONI 500 TAIFA STARS WAKIFUZU AFCON


    WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dk. Pindi Chana amesema Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 endapo timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) itafuzu kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Barani Afrika (AFCON) mwaka 2024 nchini Ivory Coast.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20,2023 jijini Dar es Salaam ambapo amesema Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma ataongoza Watanzania wa hapa nchini na waishio nchini Misri kuishangilia Taifa Stars.
    "Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi kuishangilia  Taifa Stars katika mchezo wa tarehe 24, Machi 2023 dhidi ya Uganda (The Cranes)  ambao utakaochezwa  katika mji wa Isimailia nchini Misri na mchezo wa marudiano utachezwa Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamini Mkapa" amesema Mhe. Chana.
    Aidha, amewataka wadau wa mchezo huo ikiwemo Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na mashabiki kumuunga mkono Kocha wa Timu hiyo, Adel  Amrouche, huku akiwasistiza wachezaji wajitume ili waweze kufanya vizuri katika nashindano hayo.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI YAWAAHIDI SH MILIONI 500 TAIFA STARS WAKIFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top