MSHAMBULIAJI wa Simba, Pape Ousmane Sakho amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Senegal kwa ajili ya mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Msumbiji Machi 24 Uwanja wa Olimpiki Jijini Dakar, Senegal.
Nyota wengine wa klabu za Ligi Kuu wameitwa pia na timu zao kwa ajili ya michezo ya kufuzu AFCON wiki ijayo akiwemo kinara wa mabao na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele aliyeitwa kikosi cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Wengine wa Simba walioitwa ni Hennock Inonga (DRC), Clatous Chama (Zambia) na Saido Ntibanzokiza (Burundi).
Kwa Yanga wameitwa Kipa Djigui Diarra (Mali), Khalid Aucho (Uganda), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso), Kennedy Musonda (Zambia) na Fiston Kalala Mayele (DRC).
Kutoka Azam FC wameitwa Ali Ahmada (Comoro) na Kenneth Muguna (Kenya), wakati KMC wameitwa Emmanuel Mvuyekure na Steve Nzigamasabo (Burundi) na Coastal Union ameitwa kipa Justin Ndikumana (Burundi).
Aidha kutoka Singida Big Stars ameitwa Meddie Kagere kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment