WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya Arsenal leo yamefungwa na Gabriel Martinelli dakika ya 28, Bukayo Saka mawili dakika ya 43. Ana 74 na Granit Xhaka dakika ya 55, wakati la Crystal Palace limefungwa na Jeffrey Schlupp dakika ya 63.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 69 katika mchezo wa 28 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi nane zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambayo imecheza mechi 27, wakati Crystal Palace inabaki na pointi zake 27 za mechi 28 nafasi ya 12.
0 comments:
Post a Comment