• HABARI MPYA

        Tuesday, March 21, 2023

        RONALDO AITWA TIMU YA TAIFA URENO KUFUZU EURO


        KOCHA mpya wa Ureno, Roberto Martínez amemjumuisha Cristiano Ronaldo (38) kwenye kikosi chake kwa ajili ya kufuzu Euro dhidi ya Liechtenstein Machi 23 huko Luxembourg.
        Hii itakuwa kazi ya kwanza kwa Roberto Martínez tangu achukue nafasi ya Fernando Santos baada ya fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar walipotolewa na Morocco kwa kuchapwa 1-0 Desemba 10, mwaka jana. 
        Ronaldo, ambaye kwa sasa anachezea Al-Nassr ya Saudi Arabia anataka kutanua rekodi yake ya mabao timu ya taifa kutoka 118 ya sasa kupitia mechi hizi za Kundi J kufuzu Euro ambalo wapinzani wao wengine ni Bosnia-Herzegovina. Iceland na Slovakia.

        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: RONALDO AITWA TIMU YA TAIFA URENO KUFUZU EURO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry