TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Fulham FC leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
Haukuwa ushindi mwepesi, kwani Fulham walitangulia kwa bao la dakika ya 50 la Aleksandar Mitrović, kabla ya Man United kutoka nyuma kwa mabao ya Bruno Fernandes dakika ya 75 kwa penalti na 90 na ushei akimalizia pasi ya Fred na Marcel Sabitzer dakika ya 77.
Sasa Man United watakutana na Brighton & Hove Albion katika Nusu Fainali Aprili 22, wakati Manchester City itamenyana na Sheffield United Uwanja wa Wembley Jijini London.
0 comments:
Post a Comment